Awamu ya inne ya mpango ‘‘ Udhamini wa mafunzo ya Cinéma kwa ajili ya mabadiliko’’ imezinduliwa leo Alhamisi novemba 16, 2023 na shirika lisilo kuwa la kiserekali Accountability Lab DRC.
Mpango huo, unahusu kuwapa mafunzo vijana kati ya umri wa miaka 18 na 35 ambao wanapendeleya kujifunza mambo ya cinema piya wanaotaka kuchangiliya ili kuleta mabadiliko katika jamii yao.
Baada ya kujifunza, vijana hao, wanazaminiwa na shirika Accountability lab ili kutengeneza filamu za dakika fupi zitakazo saidiya katika uhamasishaji wa jamii katika secta ya uongozi bora inchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Accountability Lab DRC inatoa fursa hii kwa vijana kutoka mikoa miwili ya nchi ambazo ni Kivu Kaskazini na Kusini zikiwa eneo ambapo mpango « Film Fellow Ship » inatekelezwa.
» Mpango huo unawapa vijana uwezo kipesa katika majifunzo, piya udhamini katika harakati zote za kutengeneza filamu zao, Wanao toka inje ya mji wa Bukavu, hugaramiwa sehemu ya kulala, chakula na Usafiri wao, wakati wote wa mpango » ndivyo zimetaja duru zetu.
Ni hadi Desemba 10, 2023 ndiyo kandideti zinachukuliwa kupitiya link hii : https://shorturl.at/dkryW
Laisser un commentaire